Ingia / Jisajili

Hii Ni Karamu

Mtunzi: Alex Rwelamira
> Mfahamu Zaidi Alex Rwelamira
> Tazama Nyimbo nyingine za Alex Rwelamira

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Alex Rwelamira

Umepakuliwa mara 76 | Umetazamwa mara 146

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Hii ni karamu ya Bwana Yesu anatuita ni karamu yenye heri na uzima wa milele X2

Mwili wake ni chakula na damu yake ni kinywaji tujongee meza yake (Bwana) kushibisha roho zetu anatualika sote kwa karamu takatifu X2

1. Yesu mwenyewe anatulisha mwili wake mwili wake ni chakula kinachoshibisha roho zetu

2. Yesu mwenyewe anatunywesha damu yake damu yake ni kinywaji safi cha uzima wa milele

3. Tukampokee hakika Yesu yupo hapa ni mzima katika maumbo haya ya mkate na divai

4. Tukampokee kwa imani na kwa uchaji anatujalia neema ya utakaso nafsini mwetu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa