Ingia / Jisajili

Kristu Alijinyenyekeza

Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma | Matawi

Umepakiwa na: Basil Tumaini

Umepakuliwa mara 2,576 | Umetazamwa mara 6,418

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KRISTU ALIJINYENYEKEZA Mtunzi: Dr. Basil Tumaini (0767847258)

Kiitikio:

Kristu alijinyenyekeza, akawa mtii, hata mauti ya msalabani.

Viimbizi:

  1. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina.
  2. Alibebeshwa msalaba, akaanguka mara tatu, kwa ajili ya dhambi zetu.
  3. Akapigwa mijeledi, akavishwa na miiba, kwa ajili ya dhambi zetu.
  4. Wakamvisha vazi la zambarau, wakamdhihaki kama mfalme, kwa ajili ya dhambi zetu.
  5. Wakamsulubisha na wahalifu, wakagawana mavazi yake, kwa ajili ya dhambi zetu.
  6. Aliposema naona kiu,wakamnywesha siki chungu, kwa ajili ya dhambi zetu.
  7. Uchungu mkali kama upanga, ukapenya moyo wa Maria, kwa ajili ya dhambi zetu.
  8. Wakamchoma ubavuni kwa mkuki, ikatoka damu na maji, ili sisi tukombolewe.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa