Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 2,694 | Umetazamwa mara 6,108
Download Nota Download MidiNINAKUPENDA
Wimbo wa Ndoa
Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
Kiitikio:
Ninakupenda mpenzi wa moyo wangu, mimi nimekuchagua twende tukaishi wote. [ X 2]
Mimi nimekuchagua katika dunia hii, Mungu na ayabariki maisha yetu. [ X 2]
Viimbizi:
1. Yesu atuambia: Mungu alounganisha, mwanadamu kamwe asijaribu kutenganisha.
2. Katika maisha yenu, katika shida na raha, mdumu, mmeungana, mu mwili mmoja sasa.
3. Iweni waangalifu, Sala mzisali sana; shetani asije kwenu kwa hila akawashinda.
4. Kwa Malezi ya Kikristu wanenu muwaongoze, mfano muangalie Familia Takatifu.
5. Upendo, uvumilivu, juhudi, uaminifu, view ndizo zenu nguzo katika maisha bora.
6. Kamwe msiukubali uovu wa siku hizi, dumuni katika yale Mafundisho yake Mungu.
7. Ulevi, uasherati, ugomvi nayo mengine, kwa Jina /Jina la Yesu nayo yapate kushindwa.