Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 1,319 | Umetazamwa mara 4,643
Download Nota Download MidiSALAMU MAMA MWEMA MARIA
Wimbo kwa Mama Bikira Maria
Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
KIITIKIO
Salamu mama mwema Maria.
Bikira pia mama, Maria.
Sisi wanao twaja mnele yako mama:
Utuombee, utuombee mama kwake mwanao Yesu Kristo (Ee Mama)
Ili tufike kwake Mungu juu Mbinguni. X 2
MASHAIRI
1. Salamu Mama Maria tunakuomba
Utuombee kwa mwanao Yesu Kristu.
Salamu Mama Mtakatifu Mama wa Mungu
Utuongoze na sisi tufike Mbinguni.
2. Salamu Mama Maria tunakuomba
Utuopoe siku zote hatarini.
Salamu Mama Chombo Bora cha Ibada
Utuombee kwa mwanao Yesu Kristu.
3. Salamu Mama Maria tunakuomba
Utuombee sisi tulio wakosefu.
Salamu Mama maria mlango wa Mbingu
Usituache saa ile ya kufa kwetu.