Ingia / Jisajili

Enyi Taifa La Mungu (Njoni Tumshukuru)

Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Basil Tumaini

Umepakuliwa mara 1,794 | Umetazamwa mara 2,596

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

ENYI TAIFA LA MUNGU NJOONI

Mtunzi: Dr. Basil Tumaini

Kiitikio: Enyi Taifa la Mungu njooni, njoni tumwimbie Mungu, njoni tumshukuru.

             Bwana ninakushukuru kwa neema zako nyingi unazonijalia Bwana asante.

Viimbizi (chagua mashairi unayotaka kuimba):

1. Na kwa uhai nilionao (Mungu wangu) kwa afya njema nakushukuru Ee Bwana Mungu asante.

2. Kwenye familia tulizonazo (Mungu wetu) Upendo wako ukatawale Ee Bwana Mungu asante.

3. Katika raha katika shida (Mungu wangu) Uko daima, u kimbilio Ee Bwana Mungu asante.

4. Kanisa lako waliongoza (Mungu wetu) Liwe imara lisimamie Ee Bwana Mungu asante.

5. Kwa Mwili wako, kwa Damu yako (Mungu wetu) Umejitoa kutushibisha Ee Bwana Mungu asante.

6. Yanatimia malengo yangu (Mungu wangu) mafanikio ninayapata Ee Bwana Mungu asante.

7. Nayo amani nchini mwetu (Mungu wetu) Tunakuomba uidumishe Ee Bwana Mungu asante.

8. Na siku hii ni kumbukumbu (Mungu wangu) Ya wema wako wewe Mwenyezi Ee Bwana Mungu asante.

9. Na kwa kinanda na matoazi (na kayamba) sauti tamu nitapaaza kukushukuru Ee Mungu.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa