Ingia / Jisajili

Kumbuka Rehema Zako

Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Basil Tumaini

Umepakuliwa mara 2,526 | Umetazamwa mara 5,106

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KUMBUKA REHEMA ZAKO

Mtunzi: Dr. Basil Tumaini

Wimbo wa katikati: Jumapili ya 26 A

Sala katika taabu

Kiitikio:

Kumbuka rehema zako Ee Bwana x 2

Mashairi:

1.    Ee Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako, uniongoze katika kweli yako na kunifundisha; maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu.

2.    Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako, maana zimekuwako tokea zamani. Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, wala maasi maasi yangu, unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako.

3.    Bwana yu mwema, mwenye adili, kwa hiyo atawafundisha njia wenye dhambi, wenye upole atawaongoza katika hukumu, wenye upole atawafundisha njia yake.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa