Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 1,255 | Umetazamwa mara 3,871
Download Nota Download MidiOMBENI NANYI MTAPEWA
Mt. 7:7-11
Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
Kiitikio:
Yesu alisema: ombeni mtapewa; tafuteni nanyi mtaona x 2
Ombeni (nanyi mtapewa)
Tafuteni (nanyi mtaona)
Bisheni mtafunguliwa
(kwa maana) (kila) aombaye hupokea,
Abishaye atafunguliwa. X 2
Mashairi: (Taz. Mt. 7:9-11 na Mt. 6:7-8).
1. Kuna mtu yupi kwenu, ambaye mwanawe akimuomba mkate, atampa jiwe?
Basi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamuombao.
2. Kuna mtu yupi kwenu, ambaye mwanawe akimuomba samaki, atampa nyoka?
Basi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamuombao.
3. Mkiwa katika sala, msipayukepayuke kama wafanyavyo watu wa mataifa;
Kwani Baba yenu anayajua mahitaji yenu kabla hamjamwomba.