Mtunzi: Dr. David S. Kacholi
> Mfahamu Zaidi Dr. David S. Kacholi
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. David S. Kacholi
Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma
Umepakiwa na: David Kacholi
Umepakuliwa mara 6,753 | Umetazamwa mara 16,031
Download Nota Download MidiKiitikio: Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha, Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha x 2.
Mashairi:
1. Wote wanionao hunicheka sana, hunifyonya wakitikisa vichwa vichwa vyao.
2. Husema alimwamini Bwana naye amwokoe, amwopoe maana apendezwa naye.
3. Kwa maana mbwa wengi wamenizunguka, kundi la waovu wamenizingira.
4. Mikono na miguu wamenitoboa, naweza kuhesabu mifupa yangu yote.
5. Wanagawanya nguo wanagawanya nguo, wapigia kura kanzu kanzu yangu.
6. Bwana usisimame mbali mbali nami, ewe msa'da wangu uje hima kunisaidia.