Ingia / Jisajili

Ndiwe Sitara Yangu

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Valentine Ndege

Umepakuliwa mara 9 | Umetazamwa mara 34

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 6 Mwaka B

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Ndiwe Sitara yangu, utanihifadhi na mateso, utanizungusha nyimbo za wokovu, nyimbo za wokovu x2 1. Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake, heri Bwana asiyemhesabia upotovu ambaye rohoni mwake hamna hila. 2. Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu, nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. 3. Mfurahieni Bwana, shangilieni enyi wenye haki pigeni vigelegele vigelegele vya furaha, ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa