Ingia / Jisajili

Nitawalisha Kondoo

Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Stanslaus Butungo

Umepakuliwa mara 1,179 | Umetazamwa mara 3,599

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

NITAWALISHA KONDOO WANGU

Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo wangu x2 Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo, nitawalisha majani mabichi ya kondeni, nitawalaza ase-ma Bwana x2

1. Ole wenu wachungaji wa Israeli, mnawatafuna kondoo walionona, na kuwatawanya mbali na zizi langu, Kwasababu hiyo asema Bwana, nitawaachisha kuwalisha kondoo, nami nitawachukua kondoo wangu

2. Mimi ndimi mchungaji mwema, mchungaji mwema hutoa uhai wake, kwa ajili ya kondoo wake, mtu wa mshahara huwaacha kondoo, pale amwonapo mbwa mwitu mkali, ambaye huwararua na kuwatawanya

3. Mimi ndimi mlango wa kondoo, ajaye kwangu kamwe hapotei, naye ataona, ataona malisho te-le


Maoni - Toa Maoni

kerbin Nov 12, 2020
wimbo mzuri sana umenigusa moyo wangu kabisa ....mtunzi endelea kutunukiwa tungo nzuri kama hizo....

Toa Maoni yako hapa