Mtunzi: Reuben Maghembe
> Tazama Nyimbo nyingine za Reuben Maghembe
Makundi Nyimbo: Anthem | Mwaka Mpya | Noeli | Pasaka | Tenzi za Kiswahili
Umepakiwa na: Reuben Maghembe
Umepakuliwa mara 1,069 | Umetazamwa mara 3,194
Download Nota Download MidiKIITIKIO
Njoni waumini (njoni nyote), njoni waumini (njoni) sote tumwimbie Mungu wetu. Tucheze (na) ngoma za kikwetu tutangaze sifa zake *2
Tucheze tamaduni zetu njoni watu wa nchi zote tumwimbie Mwokozi wetu
Malaika wa mbinguni wanaimba kwa shangwe kuu aleluya, aleluya watu wote pigeni makofi kwa shangwe tumwimbie Mwokozi wetu*2
MASHAIRI
1. Aleluya aleluya tuimbe sote aleluya aleluya, aleluya tutazitangaza sifa zake
2. Wanyama wote wa nchi na wa maji, na waushangilie utukufu wa Mungu kwa maana yeye ndiye Muumba vyote
3.Wafugaji na wakulima wa mazao yote walisifu jina lake Bwana. Wafanyakazi matajiri na wafanya biashara walitangaze jina lake
4. Ndege wa angani wanaruka, kutangaza utukufu wa Muumba wetu na ukamilifu wa neno lake aleluya
5.Makabila yote na yamtukuze mwenye enzi kwa vinubi, kwa vinanda na kwa ngoma za asili na kengele