Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 749 | Umetazamwa mara 3,342
Download Nota Download MidiSALA YA WATOTO WACHANGA
(Kuomba Uhai. Kupinga utoaji mimba.)
Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini (0767847258)
April, 2007 Manzese DSM.
Kiitikio
Ee Mungu utuhurumie
tunaangamizwa kabla hatujazaliwa.
Binadamu wanatoa mimba (wala) hawatuachi tukutumikie wewe Muumba wetu.
Ibadilishe mioyo yao (twaomba) utupiganie Ee Mungu mwokozi wetu.
Viimbizi
1. Kama ninyi muishivyo na sisi tunatamani kuishi;
mbona mnatunyang'anya zawadi ya Mungu?
2. Hebu fikiria: kama na wewe yangalikukuta haya;
Mungu alipenda nasi tumtumikie.
3. Sisi mlishatuua, wenzetu muwaonee huruma;
wengine tulitumwa kuutibu UKIMWI.
4. Ni watoto wangapi wamekwishatupwa jalalani?
Je, mnaichezea kazi yake Mungu?