Ingia / Jisajili

Wanawali Kumi

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 2,453 | Umetazamwa mara 7,539

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mathayo 25:1-13.

Ufalme wa mbinguni umefanana na wanawali kumi waliotwaa taa zao \\: wakatoka kwenda kumlaki, wakatoka kwenda kumlaki, kumlaki bwana harusi, kumlaki bwana harusi x2//. Basi kati ya hao kumi, watano kati yao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa wenye busara. Basi wale wapumbavu walizitwaa taa zao wakasau mafuta bali wale wenye busara walitwaa mafuta vyomboni mwao. Hata bwana harusi alipokawia kufika wote walikuwa wamelala (usingizi), \\: wote walikuwa wamelalax2// Mnamo usiku wa manane pakawa na kelele (pakawa) pakawa na kelele, pakawa na kelele mnamo usiku wa manane : \\[haya] tokeni muende kumlaki bwana harusi, tokeni muende kumlaki bwana harusi, tokeni muende kumlaki bwana harusix2// Basi wakaondoka wanawali wote kumi, wakaenda kuzitengeneza zile taa zao ili wapate kumpokea bwana harusi. Hapo ndipo wale wanawali wapumbavu wakawaomba mafuta wale wenye busara kwa maana taa zao zilikuwa zikizimika, lakini wale wenye busara wakawajibu hatuna mafuta ya kututosha sisi na ninyi, hatuna mafuta ya kututosha sisi na ninyi [Basi] nendeni mkanunue ya kwenu. Nao walipokwenda kufata mafuta, bwana harusi akaja wangali dukani, lakini harusi ikaendelea na mlango ukafungwa. Hata waliporudi kutoka dukani wakamuomba bwana harusi awafungulie mlango, wakamuomba bwana harusi awafungulie mlango. Hapo ndipo bwana harusi akawajibu akisema;\\ Amin, Amin, Amin nawaambieni Siwajui ninyi, siwajui ninyi, Amin nawaambieni siwajui ninyi x2//. \\Basi kesheni mkiomba, basi kesheni mkisali kwani hamjui siku wala saa ambayo bwana harusi atakapokuja x2//


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa