Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 2,887 | Umetazamwa mara 8,701
Download Nota Download MidiBass: Nani wa kunielezea muziki maana yake nini? (ni nani),
Tutti: Nani wa kunielezea maana halisi ya muziki (x2).
Bass + Tenor : Nani aweza niambia maana halisi ya muziki, nani aweza niambiamuziki kazi yake ni nini?
Tutti: Tafadhali nielezeni mwenzenu nipate kuelewa. Muziki waweza kuwa furaha kwani hufurahisha moyo, ama waweza kuleta huzuni kwani huhuzunisha nafsi, muziki hugusa kila nyanja katika maisha yetu, muziki ni lugha ya pamoja inayounganisha watu wote. Unaunganisha mataifa mbalimbali toka kila pande ya dunia, wawaunganisha bila kujali itikadi walizo nazo. Huu ndio muziki, basi njoni wote tuufurahie, enyi mataifa njoni tuunganishwe na huu muziki, Afrika na Asia (Esya) njooni tuongee lugha moja,Marekani na Ulaya njoni tuunganishwe na huu muziki.
Do ti do rf do ti, mi re mi fah mi re so fa so la la so so, so fa mi re mi fa mi re do ti do re do ti la so la ti do re do do..