Maneno ya wimbo
Ni wakati wa kubarikiwa, twendeni tutoe tulichoandaa.
Waamini, huu ndio wakati, wa kumtolea Muumba wetu.
Waamini, twendeni wote, tukatoe sadaka, Sadaka safi na nzuri tulioandaa.
sadaka ilio siri, sadaka iliyo siri, siri ya moyo na Muumba wetu. Sadaka; sadaka iliyo siri, sadaka iliyo siri, siri ya moyo na Muumba wetu.
1.Sadaka ya Ibrahimu ya kumtoa Isaka, ilikua siri ya moyo wa Ibrahimu, tuzitunze nadhiri zetu tunazoweka kwa Mungu, ili tupokee baraka za Muumba wetu.
2.Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, hamtapata thawabu asema bwana, Basi tutoapo sadaka tusipige panda mbele yetu, kama wanafiki ili watukuzwe na watu.
3.Basi sisi tutoapo sadaka hata mkono wetu wa kushoto, usijue ufanyalo mkono wetu wa kuume, Sadaka yetu iwe siri na Baba yetu wa mbinguni aonaye sirini atatujaza zaidi.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu