Ingia / Jisajili

Asante -Tumejazwa

Mtunzi: Cyprian D. Alphayo
> Mfahamu Zaidi Cyprian D. Alphayo
> Tazama Nyimbo nyingine za Cyprian D. Alphayo

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: Cyprian Alphayo

Umepakuliwa mara 44 | Umetazamwa mara 70

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Utangulizi: Tunakushukuru Mungu, tuliomba kwa Imani yetu haba, tukiwa na mashaka sana Hatukujua kwamba tutapewa na ziada, tena na ziada kubwa Hata ulipofika wakati wako wa kujibu maombi, tuliona ni muujiza Tulipoona kwamba tumepewa na ziada, tena na ziada kubwa Kiitikio: Ni neema, hakika tumebarikiwa Bwana asante (umenena) Umenena tumesikia, Asante (umetulisha) Umetulisha mwili wako Bwana asante na damu yako azizi, Tumejazwa, tumefurika tele asante x2 Mashairi: 1.Umeandaa mez mbele yetu, machoni pa wa-tesi wetu, umetupaka mafuta vichwani mwetu, na vikombe vyetu vimejazwa tena vimefurika. 2.Na sio kwamba sisi ni wema sana zaidi yaw engine, ni neema, wewe Mungu wetu haubagui, hunyeshea mvua kwa watu wote bila ubaguzi 3.Umetupenda, penda upeo, upendo wa agape tumeupata, wewe ni Mungu, si mwanadamu, haushindwi lolote, unaweza yote muumba wav yote Hitimisho: Tumejazwa, tumefurika tele asante x 3

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa