Mtunzi: Michael Matai
> Mfahamu Zaidi Michael Matai
> Tazama Nyimbo nyingine za Michael Matai
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: Michael Matai
Umepakuliwa mara 1,249 | Umetazamwa mara 3,880
Download NotaAleluya, Aleluya!
Vijilia ya Pasaka.
1. Mshukuruni Bwana kwakuwa ni mwema, Kwamaana fadhili zake ni za milele/ Israeli na aseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele.
2. Mkono wa kuume wa Bwana umetukuka, mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu/ Sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana.
3. Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni/ Neno hili limetoka kwa Bwana, nalo ni ajabu machoni petu!
Dominika ya Pasaka.
Kristu pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka/ Basi na tuifanye karamu katika Bwana.
Dominika za kawaida.
1. Nena Bwana, kwakuwa mtumishi wako anasikia/ Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
2. Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ayatie nuru macho ya mioyo yetu/ ili tujue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo.