Ingia / Jisajili

Mrudieni Mungu

Mtunzi: Wachira Sammy
> Mfahamu Zaidi Wachira Sammy
> Tazama Nyimbo nyingine za Wachira Sammy

Makundi Nyimbo: Kwaresma

Umepakiwa na: Samuel wachira

Umepakuliwa mara 192 | Umetazamwa mara 592

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Nirudieni kwa moyo wote asema Bwana Mungu mwenyezi, msirarue mavazi yenu kwa huzuni, asema Bwana nirudieni wa kufunga kuomboleza na kwa kulia (bali nasema nirudieni kwa moyo wenye toba) x2

  1. Mungu wetu mwenyezi, ni Mungu mwenye huruma, anasamehe dhambi tukimrudia yeye,

(Tuwe na moyo wenye huruma kwa watu wenye shida) x2

2.      Walishe wenye njaa wanyweshe wenye kiu, na Mungu wa huruma atakubarikia (tuwe na moyo wenye huruma kwa watu wenye shida) x2

3.      Wazike wale wafu, tembelea wagonjwa na Mungu wa huruma atakubarikia     (tuwe na moyo wenye huruma kwa watu wenye shida) x2

4.      Wavishe walo uchi, tembelea wagonjwa, na Mungu wa huruma atakubarikia, (Tuwe na moyo wenye huruma kwa watu wenye shida) x 2


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa