Ingia / Jisajili

Mtumainie Mungu

Mtunzi: Wachira Sammy
> Mfahamu Zaidi Wachira Sammy
> Tazama Nyimbo nyingine za Wachira Sammy

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Samuel wachira

Umepakuliwa mara 403 | Umetazamwa mara 1,702

Download Nota
Maneno ya wimbo

1.      Wacha kuhangaikia maisha yako mtumainie Mungu atashughulikia.

msiwe na wasiwasi juu ya chakula wala juu ya mavazi mtakayo valia.

Kweli Mungu ni mwema Bwana anayetujalia (kweli Bwana) ahadi zake Bwana kweli ni za milele x2 uzima wako uzima kweli ni bora sana, na mwili wako ni bora kuliko mavazi.(kweli Mungu ni mwema Bwana anayetujalia (kweli Bwana)  ahadi zake Bwana kweli ni za milele) x2

2.      Chukueni kwa mfano kunguru hawapandi hawavuni hawana ghala lakini Mungu anawalisha, ninyi mnao dhamani kuliko ndege.

 

3.      Angalieni na pia maua hayafanyi kazi wala hayasokoti nawaambieni Solomoni hakuuvikwa vizuri kama maua.

 

4.      Mungu huvika vizuri majani ambayo leo yako na kesho yatupwa, mkimwamini atawavika vizuri kweli zaidi ya vitu vyote.

 

5.      Basi msivurugike akili zenu mkijihangaisha juu ya mambo haya mtakula nini, mtakunywa nini; hawa ni watu wasiomjua Mungu, tafuteni kwanza ufalme wake Mungu hayo mengine yote mtapewa tu kwa ziada.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa