Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Shukrani | Zaburi
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 6,556 | Umetazamwa mara 14,608
Download Nota Download MidiKiitikio:
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, nitakushukuru kwa moyo wangu wote, mbele ya Miungu nitakuimbia zaburi. Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, nitalishukuru jina lako kwa ajili ya fadhili zako, kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako.
Mashairi:
1. Nilipokulilia Ee Mungu, ulinijibu, wewe bwana ulinijibu, ulinijibu nilipokulilia.
2. Wafalme wa dunia watakusifu kwakuwa wamesikia maneno yako.
3. Ndipo wataimba sifa za matendo yako kwa maana utukufu wako ni mkuu, mkuu sana.
4. Ee Mungu, Ee Mungu utatimiza yote uliyoahidi, fadhili, fadhili, fadhili zako zikae nasi daima.