Mtunzi: Thomas G. Mwakimata
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas G. Mwakimata
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Pasaka | Zaburi
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 3,131 | Umetazamwa mara 7,370
Download Nota Download MidiEe Bwana Mungu wangu nalikulilia ukaniponya, Ee Bwana nalikulilia ukaniponya x 2:
Mashairi:
1 (a) Ee Bwana nitakutukuza kwa maana umeniinua, wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.
1 (b) Umeniinua nafsi yangu ee Bwana, nafsi yangu kutoka kuzimu.
2 (a) Umeniuhisha na kunitoa, miongoni mwao washukao shimoni.
2 (b) Mwimbieni Bwana, mwimbieni zaburi, enyi watauwa watauwa wake.
3 (a) Nakufanya shukrani kwa kumbukumbu, kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
4 (a) Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, katika radhi yake mna uhai.
5 (a) Huenda kilio huja kukaa usiku, lakini asubuhi huwa furaha.
3 (b) Ee Bwana usikie unirehemu, Bwana uwe msaidizi wangu.
4 (b) Uligeuza matanga yangu kuwa machezo, Ulinivua gunia ukanivika furaha.
5 (b) Ee Bwana Mungu wangu ee Mungu wangu, Ee Bwana nitakushukuru milele.