Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini
> Mfahamu Zaidi Dr. Basil B. Tumaini
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Basil B. Tumaini
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 776 | Umetazamwa mara 3,018
Download Nota Download MidiNJONI NANYI MTAONA
(Yn. 1:38-39)
Wimbo wa Wito
Mtunzi: Dr. Basil B. Tumaini (+255 767 847 258)
KIITIKIO
Yesu alipogeuka akawaona wakimfuata. Naye akawaambia, “mnatafuta nini?”
Wakamwambia,
“Rabi (Mwalimu), x 2
Wewe unakaa wapi?”
Naye Yesu akawaambia,
“Njoni, nanyi mtaona.”
Wakaenda wakaona akaapo, nao wakakaa kwake siku ile. X 2
VIIMBIZI
1. (Mt. 10:16) Ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Iweni werevu kama nyoka, iweni wapole kama njiwa.
2. (Mt. 10:7) Mkahubiri: “Ufalme wa Mungu Umekaribia”. Fukuzeni pepo, poozeni magonjwa, wahubirini habari njema.
3. (Lk. 10:20) Msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii, bali kwa kuwa majina yenu yameandikwa Mbinguni.
4. (Taz. Yn. 13:37 na Yn. 6:67-68) Tuwe tayari kuutoa uhai kwa ajili ya Kristo/
“Twende kwa nani, Wewe unayo maneno ya Uzima wa Milele.”