Ingia / Jisajili

GHARAMA YA WOKOVU

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 324 | Umetazamwa mara 1,568

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
GHARAMA YA WOKOVU 1.Kumbukeni upendo wake Mungu wetu waku mtoa mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele, -tuzishike amri zake tuepuke malumbano majirani tupendane kama alivyotupenda Mungu pokea shukurani zetu Mungu (wetu) wanao tunakupa sifa Mungu (wetu) twatangaza matendo yako bila (hofu) twasimulia sifa zako, maana wewe wastahili kutukuzwa wewe Mungu wastahili kuheshimiwa Tunaimba (imbaimba) hata na kucheza twashukuru Mungu kwa upendo wake, tunavipiga vinanda vyetu twavumisha sifa zako Ee Mungu x2. 2.Damu iliyomwagika msalabani ndiyo gharama ya wokovu wetu mzigo wa dhambi alituondolea madeni yetu aliyalipa yote, 3.Taji la miiba walimvisha kwa nguvu wakampiga mijeledi bila huruma, yote aliyavumilia Bwana wetu ili tupate uzima wa milele, MWISHO Kama haingekuwa ni (1.neema zako, 2.huruma yako, 3.upendo wako) hatungefika hapa siku ya leo twakushukuru Baba twasema asante, asante Baba asante ‘sante kwakutuokoa kutoka dhambini twakushukuru Baba twasema ‘sante x3 asante asante asante sana, Baba asante (asante) kwa upendo wako (asante) na fadhili zako (asante) mimi nashukuru, uligharamika (asante) ili niupate (asante) wokovu huu (asante) mimi nashukuru, ulifadhaika (ee Bwana) na kusononeka (ee Bwana) kwa ajili yangu (ee Bwana) Bwana mimi nashukuru ,gharama ya wokovu (ee Bwana) ni kubwa mno (ee Bwana) tena haielezeki (ee Bwana) mimi nashukuru, Baba { asante kwa pendo kwa pendo pendo twasema asante asante Baba} x4.

Maoni - Toa Maoni

Ingudia Moses Mar 03, 2024
Kazi smart big bro

Toa Maoni yako hapa