Ingia / Jisajili

SIMAMENI TUPELEKE

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 643 | Umetazamwa mara 1,471

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
SIMAMENI TUPELEKE Simameni waumini wote tupeleke vipaji vyetu vyote kwake Muumba kwani mali yake x2 Baba (tumebeba mali yetu tunaleta kwa furaha twakuomba Mungu mwenye enzi uipokee, ni mapato ya kifedha ni mazao ya mashamba tunaleta kwako Baba ili utubariki ) x2. 1.Sadaka ni mapato Baba uliyotujalia, nasi tunaileta kwako kama shukrani yetu, twakuomba Mwenyezi uipokee leo, mikononi mwa padre sadaka yetu hii, kisha utubariki kwa Baraka ya-ko, na ile yake mwana, na ya Roho Mtakatifu. 2.Maisha mazuri Baba sisi tunajivunia, afya njema ya mwili na roho pia umetupa, basi tunajileta kwako kama dhabihu, hivyo ikupendeze kwani ni mali yako, Ba-ba twakuomba utupokee- leo, na kisha utubariki tuende tumetakasika. 3.Tunapoleta mapato haya Baba twatimiza, wajibu wetu kwako na pia kwa kanisa letu, Baba twafurahia mapendo yako kwetu, pia tunashukuru kwa Baraka za-ko, na sasa twakuomba uwatembe-lee, wasiojiweza nao ukawabariki. 4.Tunawaombea wale wenye mioyo migumu, wasiopenda kutoa zako ya mapato yao, uwatumie Roho yule msaidizi, ili awakumbushe majukumu ya-o, yakuleta chakula kwa nyumba ya-ko, na kujenga kanisa kanisa lako wewe.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa