Maneno ya wimbo
MTETEZI
1.Nakumbuka zamani zangu nilipokuwa kitoto kichanga sikuwa na uwezo wala nguvu zangu mimi, nilikuwa ni mnyofu na mnyenyekevu sana lakini hata ndege, hangenikaribia, kwa kuwa mtetezi Mungu yupo, kwa kuwa mtetezi wetu yupo leo,
Imbeni sifa zake Mungu (wetu) tukuzeni jina lake (yeye) yeye (ndiye) pekee yake anastahili sifa (Mungu) enzi pia na utukufu, vyote ni vyake hata milele x2
2.Mipango yao maasidi ni kuweka nyua imara mbele yako ili wewe upate kutaabika maishani, unapopanga mambo yako wao washakupangulia lakini usihofu,
wala usitikisike, kwa kuwa mtetezi Mungu yupo, kwa kuwa mtetezi wetu yupo leo,
3.Dunia imekua janga masaibu chungu nzima mbele yetu wakristu tusikate tamaa kamwe ya kuishi, magonjwa ya kila namna nchi na nchi kupigana lakini tuwe dhabiti, katika imani yetu, kwa kuwa mtetezi Mungu yupo, kwa kuwa mtetezi wetu yupo leo,
MWISHO
-Chombo chetu ki salama kinaelea majini hehe - mawimbi yanapotupiga dhoruba inapotupiga sisi tuna mtetezi, Imani yetu twaiweka kwake nahodha mkuu hehe - dunia ikitusaliti, tusisahau wateule kwamba tuna mtetezi (wetu Mungu) tuna mtetezi (atupenda) tuna mtetezi
Magonjwa yakikulemea - kumbuka unaye mtetezi, dakitari yuataka hongo – kumbuka unaye mtetezi, Mwajiri akikudhulumu - kumbuka unaye mtetezi, kazini hautakikani - kumbuka unaye mtetezi, Marafiki wakikutenga - kumbuka unaye mtetezi, mikutanoni hukupinga - kumbuka unaye mtetezi, kumbuka unaye mtetezi, ni Mungu mtetezi wako daima mpe sifa zote leo..
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu