Ingia / Jisajili

Mungu Ni Yule Yule

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 571 | Umetazamwa mara 1,484

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
MUNGU NI YULE YULE MWANZO Mungu ni yule -Mungu ni yule, jana na leo - na milele, Mungu ni yule- Mungu ni yule, (Mungu ni yule yule yule) x2 Ndiye yeye Mungu mmoja (Mungu yeye ndiye) aliyekuwa ndiye yeye Mungu mmoja aliyeko, ndiye yeye Mungu mmoja (Mungu yeye ndiye) ‘takaye kuwa ndiye yeye Mungu wa kweli anaishi, ndiye yeye Mungu mmoja (Mungu yeye ndiye) wa baba zetu ndiye yeye yule Mungu, wa milele, Ni Mungu wa jana ni Mungu wa milele, Mungu wetu habadiliki (Mungu) ni yule yule jana leo na milele (Mungu) ni (ni Mungu ni) yule yule, kiangazi hata masika (Mungu) ni yule yule jana leo na milele (Mungu) ni (ni Mungu ni) yule yule, Yeye ndiye alfa na omega mwanzo na pia mwisho hakuna mwingine kama yeye, (ni yeye ndiye) Bwana wa mabwana Mfalme wa wafalme hakuma mwingine kama yeye 1.Viumbe ulivyoumba vinakutuza kwa furaha vinasifu jina lako baba, na vile hatuvioni pia vya kusifu, kwa maana wewe Mungu haubadiliki 2.Ukaumba ulimwe-ngu kwa ne-no lako, nchi kavu na bahari ukavitawanya, usiku ukawa giza mchana mwangaza, sifa zako zinadumu kwa vizazi vyote MWISHO Mungu aliyekuwa tangu mwanzo wa dunia na Mungu aliyeko sasa Mungu ni yule yule Mungu aliyeumba ulimwengu kwa masiku na Mungu aliyeko sasa Mungu ni yule yule Alliyeikomboa israeli toka misri na Mungu aliyeko sasa ni Mungu ni yule yule (ni yeye Mungu tangu mwanzo na Mungu ‘ko sasa) ni yule yule Habadiliki kamwe -Mungu ni yule yule Daima na milele -Mungu ni yule yule Aliyetukomboa -Mungu ni yule yule Na ndiye yuko sasa - Mungu ni yule yule Basi na tumwimbie -Mungu wetu nyimbo za ushindi Tumchezee kwa furaha Mungu tumsifu He na sauti tuzipaze sauti za shangwe Tumwimbie Mungu wetu nyimbo za ushindi Ho na vifijo tuvipige tumfanyie shangwe Tumwimbie Mungu wetu nyimbo za ushindi (tumpigie makofi tena makofi kwake muumba makofi Mungu atupenda ) x3 Mungu ni yule yule.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa