Ingia / Jisajili

SALAMU MAMA

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 362 | Umetazamwa mara 1,365

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
SALAAM MAMA Salamu mama bikira mwema mama Maria (mama wa Mungu) salamu mama chombo bora cha ibada, uliyejaa neema nyingi twakusalimu (mama ‘kanisa) salamu mama chombo cha kuheshimiwa {(sisi wanao leo) Tunakuimbia (twaimba) na tunakuchezea twazitaja (twataja) sifa zako mama tulia ulipo (siku zote wewe ma) tushike mkono (mama tushike) na utembee nasi (mkono pole) polepole tufikishe alipo mwana } x2 alipo mwanao Yesu. 1. S/A -Malaika Gabreli katumwa naye Mungu kumletea Maria habari njema, mama kwa mshangao kastajaabu kasema itawezekanaje kwangu bikira, T/B -Maria usiogope ni Roho usiwe na hofu, ni Mungu kakuchagua utuzalie mkombozi Yesu mama Maria… 2. S/A -Upendo wako mama hauwezi pimika malezi yako mama ni ya kipekee, mapenzi yako mama pale msalabani yalimpa mwanao ukakamavu, T/B -Maria mama wa Muumba maria malango wa mbingu maria kimbilio letu sisi wakosefu bikira mwaminifu mama Maria.. 3. S/A -Kwa sala zako mama tumekua imara usichoke daima kutuombea, safari ni ndefu yenye magumu mengi mama usituache gizani humu, T/B -Maria mwombezi wetu Maria msaada wetu Maria mwenye huruma na upendo mwingi tunakukimbilia mama Maria..

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa