Maneno ya wimbo
KILIO CHA WANAKENYA
Utangulizi
All: Woi, woi, woi Mungu Baba sikia kilio chetu x5
Eee Mungu Mwenyezi twakuomba usikie, Baba tunalia twakuomba usikie kilio cha wakenya Wanao wanaangamia nchini humu, sisi tunalia twakuomba usikie, kilio chetu Baba (kwani Baba) nchi yetu inaangamia (kwa kukosa) usalama na amani (wana wako) wanauana wao kwa wao (Mungu Baba) tunaomba utusaidie, kumaliza (Baba) vita hivi (ili) wanawako waishi kwa amani na umoja. Mungu Baba (Mungu) Mungu Mwana (Yesu) Mungu Roho Mtakatifu unaweza, hivyo Baba (yetu) imarisha (sana) usalama Kenya yetu iwe huru.
1. Ladies: Uhuru wetu Baba, haupo nasi tena, tunalia kila siku Ee Baba usituache tunapokulilia Baba utusikilize, Baba tunaomba uturejeshee Uhuru wetu Baba tunaohitaji
2. Men: Upendo wako wa ki-mungu, haupo tena kati yetu, kwani chuki imekithiri na kumea mizizi miovu hivyo tunakulilia, Baba sikia kilio chetu, Tunaomba upendo wako uenee kati yetu tupendane siku zote, kama unavyotupenda wewe
3. Ladies: Uhai wa binadamu hauheshimiwi kamwe, watu wanachinjana mithili ya hayawani Baba njoo njoo upesi utuokoe sisi wana, Kwani tumaini letu, ni kwako Maulana wewe ndiwe Mwokozi, Baba njoo hima
4. Men: Siasa za kupotosha, mafarakano mengi kaleta, ukabila ukabila umekuwa wimbo wa taifa. Ewe Mungu wa Israeli, ndiwe Mungu uliyekuwako, ewe Mungu wa Yakobo, ndiwe Mungu utakayekuwa, Basi Mungu uliyeko, tunaomba suluhisho kwa haya maswala nyeti, yanayoikumba nchi yetu
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu