Ingia / Jisajili

BADO NASUBIRI BWANA

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 735 | Umetazamwa mara 2,027

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
BADO NASUBIRI BWANA MWANZO Nakuita Bwana wangu napaza sauti nakuita Bwana nisikie, Macho yangu yapo kwako natazamia msaada wako Bwana nisikie, Basi Bwana usikawie mtumishi wako yuasubiri Bwana nisikie, Pasipo wewe (Bwana) mimi sijiwezi (Bwana) kwani mdhaifu nakuhitaji sana, uniongoze (Bwana) kwenye njia panda maana wewe ndiwe kiongozi mwaminifu (Bwana) {uniimarishe niwe mwenye nguvu niweze kuyafanya mapenzi yako, nikujue wewe tena nikupende nikutumikie siku zangu zote } x2. 1.Nilalapo hata niamkapo najiweka mbele yako Bwana, kwani (Bwana) wewe ndiwe (uliye) mlinzi wangu (mimi) Bwana, mimi (Bwana) nahitaji (sana) msaada wako maana. 2.Mahangaiko mengi ya ulimwengu yamedhohofisha nafsi yangu, Bwana (wangu ni) naomba uniepushe na haya yote, mimi (Bwana) nahitaji (sana) msaada wako maana. 3.Giza limefumba macho yangu sioni ninapokwenda mimi, Bwana (wangu ni) naomba usikawie (ee) Bwana naomba, mimi (Bwana) nahitaji (sana) msaada wako maana. MWISHO Sop- Mungu wangu na Bwana wangu – nakusubiri, Alto-nina haja na wewe Bwana – ninakusubiri, Tenor-wewe ndiwe kiongozi – nakusubiri, Bass-kwani mimi Bwana ni kipofu – ninakusubiri, wewe Bwana ni mambo yote (Bwana wangu) waifahamu kesho yangu Bwana, Bwana wangu ninaomba (Bwana wangu) usikawie kuja kwangu Bwana, mimi ninakusubiri, Bwana wangu (ee Bwana) mimi nakutegemea wewe ndiwe (ee Bwana) kiongozi mwaminifu, Bwana wangu (ee Bwana) sina wakumlilia, hivyo Bwana (ee Bwana) nasubiri jibu lako. Shida zangu nakupa wewe (wewe Bwana) maana wewe unalojibu (hakuna kamwe) hakuna linalokushinda (naamini) wewe Mungu unaweza, (machozi yangu) machozi yangu wayaona (wewe Mungu) naamini utayafuta (ninaomba) Bwana Mungu naomba nijibu, Mungu naomba nijibu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa