Ingia / Jisajili

MARIA NI MAMA

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 475 | Umetazamwa mara 1,300

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
MARIA NI MAMA Ni Maria mama, ni Maria mwombezi, ni Maria mama mzazi wa Mungu x2 (mama) Maria mama wa Mungu Maria, mzazi wa Mwokozi ni Maria, alishuhudia mateso yamwanawe,hakika anastahili kuwa mama . 1. Men:Ulimzaa Yesu Mwokozi mama, ukamleta hapa duniani mama, Ladies: (Ndipo sasa tunasema wewe ni mama, ndipo sasa twangaza, wewe ni mama) x2 aeh 2. Men:Ukombozi ulitua ulimwenguni, ulipokubali ombi la malaika Ladies: (Daima wewe ni mama, ni mama yetu, tangu sasa na milele, wewe ni mama) x2 aeh 3. Men:Malezi yako mama ni ya kipekee, yalidhihirika kwa huyo mtoto Yesu Ladies: (Hakika pokea sifa, wewe ni mama, kwa kazi uloifanya pongezi mama) x2 aeh 4. Men:Ulivumilia mateso ya mwanao, ukayaona pia na mauti yake Ladies: (Kwa kweli tunatambua, uzazi wako, sisi wana wako hapa, ulimwenguni) x2 aeh 5. Men: Mungu Mwenyezi kweli alikutambua, tangia mwanzo mpaka mwisho wa dahari Ladies: (Kwani maisha yako, yalipendeza, mwishowe ukapalizwa, mbinguni kwa baba)x2 aeh

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa