Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Moyo Mtakatifu wa Yesu
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 607 | Umetazamwa mara 2,466
Download Nota Download MidiSifa za moyo, wake Yesu (mimi) kamwe sitaacha (mimi) kamwe sitaacha kuzitaja
Maishani mwangu nitasifu nitaimba moyo, moyo wake Yesu
Ee Bwana Yesu mpendelevu twaomba rehema, sisi wakosefu
1.Kwa rehema zake nyingi ametujalia
Tumpe Bwana shukrani zetu na tu mtumikie
Nitasifu moyo – nitaimba moyo moyo wa Yesu
Ameonyesha upendo usio na kifani
Hata akakubali kutufia msalabani
Nitasifu moyo – nitaimba moyo moyo wa Yesu
2.Unamokaa hazina za hekima na elimu
Unamokaa utimilifu wake Bwana Mungu
Nitasifu moyo – nitaimba moyo moyo wa Yesu
Moyo wenye uvumilivu na huruma nyingi
Mkarimu kwa wao wote wanaokuomba,
Nitasifu moyo – nitaimba moyo moyo wa Yesu
3.Moyo unaotupatanisha na Baba yetu
Kutufanya kitu kimoja naye Baba yetu
Nitasifu moyo – nitaimba moyo moyo wa Yesu
Amani na furaha tele kweli twazipata
Wokovu wake Bwana Mungu kweli twauona
Nitasifu moyo – nitaimba moyo moyo wa Yesu