Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 1,983 | Umetazamwa mara 7,262
Download Nota Download MidiJiwe walilolikataa waashi – limekuwa jiwe kuu la pembeni
Jiwe walilolikataa waashi (jiwe hilo) limekuwa jiwe kuu
la pembeni x2
1.Kwa hiyo wekeni mbali nanyi uovu wote, na udanganyifu wote
unafiki, wivu na masingizio ya kila namna
2.Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa,
yatamanini maziwa ya kiroho (yasiyoghoshiwa ili kwa hayo mpate)
kuukulia wokovu ikiwa kweli – mmeonja ya kwamba
Bwana ni mwema Mwendeeni Yeye aliye jiwe lililo hai,
lililokataliwa na wanadamu bali – kwa Mungu ni teule na la thamani
kwake
3.Ninyi nanyi kama mawe yaliyo hai, mmejengwa kuwa nyumba ya
Roho, mpate kuwa ukuhani, mtakatifu mkitoa dhabihu za kiroho
zinazokubaliwa – na Mungu kwa njia ya Yesu Kristu