Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Noeli
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 995 | Umetazamwa mara 3,240
Download Nota Download Midi1.Leo Mfalme kazaliwa – Bwana Mtawala mbingu na nchi
Dunia ifurahi sana – Na ifanye shangwe kwa Mwokozi
Amezaliwa huko Betlehemu, pangoni zizini mwa ng'ombe, amelazwa
Na zawadi zetu twende tumwone , pia tumpigie magoti, tumwabudu
2.Ataitwa Emmanueli – Yani Mungu yu pamoja nasi
Mfalme wa dunia na mbingu – Mungu mwenye nguvu kazaliwa
3.Mleta amani kazaliwa – Kwetu sisi wana wadunia
Hii ni siku ya heri kwetu – Amani ya kweli imeshuka
4.Ni shangwe kubwa sana leo – Tumechangamka kweli kweli
Wokovu wetu watimia – Mkombozi leo kazaliwa