Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 334 | Umetazamwa mara 1,732
Download Nota Download MidiKristu Mwanakondoo wa Mungu,
Msalabani wahangaika kwa ajili yangu
Ninakiri hayo yote mimi nimesababisha,
Ninaomba msamaha nazijuta dhambi zangu
1.Mungu unirehemu Mungu unirehemu,
kwa kuwa nimetenda dhambi Mungu ’nirehemu
2.Mzigo wa dhambi zangu nimekubebesha,
na bila hatia wahukumiwa ufe Bwana
3.Umenifanya huru kwa kifo chako Bwana,
njia za shetani umenitoa nikufuate
4.Kamwe nyuma sirudi nasonga mbele mimi,
ni wajibu wangu kutimiza mapenzi yako