Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 680 | Umetazamwa mara 2,731
Download Nota Download MidiNimekukimbilia Wewe Bwana, nisiaibike milele kwa haki yako 'niponye,
Mikononi mwako Bwana naiweka roho yangu
1.Kwasababu ya watesi wangu nimekuwa laumu
Naam hasa naam hasa kwa jirani zangu
Nimekuwa kitu cha kutisha kwa rafiki zangu,
Walioniona njiani walinikimbia
2.Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa,
Nimekuwa kama chombo kilichovunjika
Maana nimesikia masingizio ya wengi,
Hofu ziko hofu ziko hofu zi’ pande zote
3.Lakini mimi ninakutumaini Wewe Bwana
Nimesema Wewe ndiwe ndiwe Mungu wangu
Nyakati zangu ee Bwana zimo mikononi mwako
’niponye na’dui zangu nao wan’onifuatia
4.Umwangaze mtumishi wako kwa nuru ya uso wako
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako
Iweni hodari hodari mpige moyo konde,
Ninyi nyote ninyi nyote mnaomngoja Bwana