Ingia / Jisajili

IYELELE AMEFUFUKA

Mtunzi: Wachira Sammy
> Mfahamu Zaidi Wachira Sammy
> Tazama Nyimbo nyingine za Wachira Sammy

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Samuel wachira

Umepakuliwa mara 1,295 | Umetazamwa mara 2,243

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Mwanzo Mkesha wa Pasaka
- Mwanzo Dominika ya Pasaka

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
 • 1. (a) Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo (jambo gani) tegeni masikio yenu niwaarifu
 •     (b) Leo asubuhi na mapema ametoka (kaburini) tumshangilie Mwokozi amefufuka.

 • Yu hai Mwokozi Yesu amefufuka, kaburini ametoka leo yu hai.
 • Dunia ishangilie na kufurahi aleluya ukombozi umetimia, tumshangilie
 • (Iyelele yelele yelele iyelele njoni tuimbe, iyelele yelele yelele iyelele Amefufuka)x2

 • 2. (a) Wayahudi walifikiria wameshinda (bali kumbe) walikuwa wamesahau alishasema
 •     (b) Atakufa na kufufuka siku ya tatu (wayahudi) waliaibika na kusema ameibiwa.
 • 3. (a) Mungu kaupenda ulimwengu hata sasa (kamtoa) mwanaye wa pekee afe msalabani
 •     (b) ili wokovu na huruma yake Mungu (Mungu wetu) zitufikie sisi watoto wake.
 • 4. (a) Yesu aliteswa kwa 'jili ya dhambi zetu (wanadamu) huu ni upendo wa pekee na wa ajabu
 •     (b) nasi tuwapende pia na ndugu zetu (na jirani) nasi tuuone upendo wa Mungu wetu.

 • Maoni - Toa Maoni

  Hakuna maoni kwenye wimbo huu

  Toa Maoni yako hapa