Ingia / Jisajili

Jivikeni Upendo

Mtunzi: Emmanuel Daniel Mutura
> Tazama Nyimbo nyingine za Emmanuel Daniel Mutura

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Emmanuel Daniel Mutura

Umepakuliwa mara 1,002 | Umetazamwa mara 3,249

Download Nota
Maneno ya wimbo

JIVIKENI UPENDO [E.D.MUTURA]

Jivikeni upendo, jivikeni, jivikeni upendo (upendo) ndio kifungo cha ukamilifu (ndio), ndio kifungo cha ukamilifu (ndio) ndio kifungo cha ukamilifu x2

  1. Basi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu upole na uvumilivu, mkichukuliana na kusameheana.
  2. Pia  mtu ye yote akiwa na sababu, ya kumlaumu mwenzake, kama Bwana alivyowasamehe ninyi nyote, vivyo hivyo na ninyi nyote vumilianeni, mkichukuliana na kusameheana.
  3. Na amani ya Kristo, iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa, katika mwili mmoja, tena iweni watu wa shukrani kwa Bwana.
  4. Neno lake Bwana likae kwa wingi, ndani yenu, katika hekima yote,mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, pia na nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu.
  5. Na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa