Ingia / Jisajili

Kinubi Kiwapi?

Mtunzi: Elijah M Kilonzi
> Mfahamu Zaidi Elijah M Kilonzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Elijah M Kilonzi

Makundi Nyimbo: Mwaka Mpya | Shukrani

Umepakiwa na: ELIJAH Mulei

Umepakuliwa mara 775 | Umetazamwa mara 1,860

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kinubi kiwapi? Leteni. Na ngoma iwapi? Leteni tumwimbie Bwana wimbo mpya. X2

(Oh! Yeye huyatenda mambo, oh! mambo makuu)x2

1. Ni Yeye aliyeumba binadamu na vitu vyote; (ni nani mwingine angeweza kutenda hayo?)x2

2. Ni Yeye katenganisha bahari na nchi kavu; (ni nani mwingine angeweza kutenda hayo?)x2

3. Ni Yeye alirebesha ulimwengu kwa mimea, (vilima, mabonde, hata wanyama mbalimbali)x2

4. Nalo anga kalipamba kwa mwenzi, nyota, mawingu, (pia jua linalotuangazia mchana)x2

5. Ni Yeye katenganisha usiku na mchana; (ni nani mwingine angeweza kutenda hayo?)x2


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa