Maneno ya wimbo
{Natwende ndugu –tutoe.x2
Sadaka zetu kwa Bwana} X2
1. Wakati sasa ndugu yangu ni kweli na umefika ,
Wa kwenda mbele ya Bwana kutoa shukrani zetu
Basi na sote ndugu tuanze kujifiki-ria
Kile tutakachokitoa kama shukrani zetu
2. Naweka mikono mifukoni naona haya kutoa
Kile ninachokipata kwani ni kidogo mno
Kweli hakiwezi kutosha kutosha wema wako Ee Bwana
Nitoe nini Mungu kitakachokukupendeza
3. Nisimamapo kwenda mbele ya Bwana kumtolea
Sadaka yangu kidogo hata pia duni sana
Ninawaona wenzangu wakitoa zao nyingi
Naona heri niketi nisiitoe kabisa
4. Tukumbukeni mjane aliyeitoa sadaka
Iliyokuwa kidogo na Bwana kaipokea
Kwa ukarimu alikitoa alichojaliwa
Ndio maana sadaka yake ilikubaliwa
5. Ee Bwana Mungu uwezo wangu kweli unaujua
Ninakuomba ee Bwana Mwenyezi Mungu pokea
Sadaka yangu ingawa ingali kidogo mno
Uipokee ee Bwana kwa mikonoyo miwili
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu