Maneno ya wimbo
Kristo Paska yetu, amechinjwa sadaka, tuile karamuye na tuimbe aleluya.
1. Aliyejitoa sadaka ya paska wakristu wamtolee sadaka ya sifa.
2. Mwanakondoo amewakomboa kondoo, Kristu asiye na dhambi amewapatanisha na Baba watu wenye dhambi.
3. Mauti na uzima vimeshindana ajabu, mkuu wa uzima aliyekufa atawala mzima.
4. Utuambie Mariamu uliona nini njiani, niliona kaburi la Kristo mzima na utukufu wa mwenye aliyefufuka.
5. Mashahidi ni Malaika, leso ya uso na mavazi, Kristo tumaini langu kafufuka awatangulia Galilaya.
6. Twajua Kristu amefufuka kweli katika wafu, ewe mfalme mshindani utuhurumie. Amina Aleluya.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu