Ingia / Jisajili

Uturehemu

Mtunzi: Cyprian D. Alphayo
> Mfahamu Zaidi Cyprian D. Alphayo
> Tazama Nyimbo nyingine za Cyprian D. Alphayo

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma | Zaburi

Umepakiwa na: Cyprian Alphayo

Umepakuliwa mara 7 | Umetazamwa mara 13

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Uturehemu Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana, Kwa kuwa tumetenda dhambi. 1.Ee Mungu unirehemu sawa sawa sawa na Fadhili zako, kiasi cha wingi wa Fadhili zako, Uyafute makosa yangu, unioshe kabisa na uovu wangu, unitakase dhambi zangu. 2.Maana nimejua mimi makosa yangu, na dhambi yangu I mbele yangu daima, nimekutenda dhambi wewe peke yako, na kufanya maovu mbele za macho yako. 3.Ee Mungu uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliotulia ndani yangu, usinitenge na uso wako, wala Roho yako mtakatifu usiniondolee. 4.Unirudishie furaha ya wokovu wako, unitegemeze kwa roho ya wepesi, Ee Bwana uifumbue midomo yangu, na kinywa changu kitazinena sifa zako.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa