Ingia / Jisajili

Leo Amezaliwa Mwokozi (Revised)

Mtunzi: Respice Makoko
> Mfahamu Zaidi Respice Makoko
> Tazama Nyimbo nyingine za Respice Makoko

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: RESPICE MAKOKO

Umepakuliwa mara 2,602 | Umetazamwa mara 7,054

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Leo, leo, leo amezaliwa Mwokozi wetu Kristu, Leo amezaliwa Bwana wetu Yesu Kristu.x2

MASHAIRI

  1. Saa sita ya usiku Malaika wa Mungu, walitoa taarifa ya kuzaliwa Bwana.
  2. Malaika wanaimba huko juu mbinguni, wafurahi kuzaliwa kwake Mwokozi wetu.
  3. Tufurahi na tuimbe tupige na makofi, vigelegele tupige Mwokozi kazaliwa.
  4. Kazaliwa mtoto Yesu kwenye hori la ng’ombe, twende sote tukamwone Bethlehemu ya Yuda.
  5. Ataitwa jina lake mshauri wa ajabu, Mungu Mfalme wa amani yuko pamoja nasi.
  6. Na uweza wa kifalme uko begani mwake, ni M-falme wa amani na Bwana wa milele.
  7. Utukufu kwake Mungu huko juu mbinguni, na amani wawe nayo wenye mapenzi mema.
  8. Twimbe sote aleluya kwa shangwe na furaha, kwani leo tumepata nuru ulimwenguni.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa