Ingia / Jisajili

Mmomonyoko wa Maadili

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 888 | Umetazamwa mara 2,265

Download Nota
Maneno ya wimbo

ORGAN. Mmomonyoko mmomonyoko wa maadili katika kanisa na katika jamii zetu, unaongezeka unaongezeka kila kukicha, siyo kwa Vijana peke yao hata kwa wazee. Simu za mkononi zimewaharibu vijana, zimewaharibu vijana wanazitumia kutazama picha za utupu. (Pombe, bangi na madawa ya kulevya, vimewaharibu vijana (na kupelekea) kufanya vitendo visivyo faa kwa jamiix2) (kama vile) wizi, pamoja na ubakaji uzinzi mauaji ya kutisha uvaaji mbaya, unyoaji wa nywele mbaya nazo ndoa za jinsia moja. Tuombe tuombe tuombe kwa Mungu, atuhurumie makosa yetu, atuogoze kuamua na kutenda kwa adili. Mabinti nao wanavaa nusu uchi wakionesha utupu wao, wanazichubua nyuso kwa vipodozi vikali wamkosoa Muumba wao, wakisha kubeba mimba tena kwa hiari yao bila huruma wanazitoa, wazaapo watoto waliopewa na Mungu wanawatupa majalalani, wengine wanaongeza sehemu za miili yao kwa sababu ya uasherati, wapo wanaokimbia maisha mazuri kwao kwenda kujiuza mitaani. (Tuombe, tuombe tuombe kwa Mungu atuhurumie makosa yetu, atuongoze kuamua na kutenda kwa adili x2.). (Kwenye familia zetu, ndiko maadili yanakozaliwa, inasikitisha, kuwa ndiko unakoanzia mmomonyoko wa maadili x2). Baba ni mlevi kila siku ashinda baa arudipo ugomvi ndani, tena ananyumba ndogo, maadili yatajengwa na nani? Mama vivyohivyo kila siku kwa majirani watoto alionao ila mtoto na baba yake, maadili yatajengwa na nani?. (Tuombe, tuombe, tuombe kwa Mungu atuhurumie makosa yetu, atuongoze kuamua na kutenda kwa adili x2.)


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa