Ingia / Jisajili

Nasadiki (The Nicene Creed)-Credo-Misa Ya Maserafi

Mtunzi: Cyprian D. Alphayo
> Mfahamu Zaidi Cyprian D. Alphayo
> Tazama Nyimbo nyingine za Cyprian D. Alphayo

Makundi Nyimbo: Anthem | Mafundisho / Tafakari | Misa

Umepakiwa na: Cyprian Alphayo

Umepakuliwa mara 126 | Umetazamwa mara 486

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi, Muumba mbingu na nchi, na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, Nasadiki kwa Bwana Mmoja Yesu Kristo, mwana wa pekee wa Mungu, aliyezaiwa kwa Baba tangu milele yote, Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli, aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba, ambaye vitu vyote vimeumbwa naye. Ameshuka toka mbinguni, kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu. Akapata mwili kwa uwezo wa Roho mtakatifu, kwake yeye bikira Maria akawa mwanadamu.Akasulubiwa pia kwa ajili yetu sisi, akateswa kwa mamlaka ya ponsio pilato, akafa, akazikwa, akafufuka siku ya tatu kadiri ya maandiko, akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Baba, atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu, nao ufalme wake hautakuwa na mwisho, Nasadiki kwa Roho mtakatifu, Bwana mleta uzima, atokaye kwa Baba na mwana, anayeabudiwa na kutukuzwa, Pamoja na Baba na mwana, aliyenena kwa vinywa vya manabii. Nasadiki kwa kanisa moja, takatifu, katoliki la mitume, naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi, nangojea na ufufuko wa wafu, na uzima wa milele ijayo Amina.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa