Mtunzi: Cyprian D. Alphayo
> Mfahamu Zaidi Cyprian D. Alphayo
> Tazama Nyimbo nyingine za Cyprian D. Alphayo
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: Cyprian Alphayo
Umepakuliwa mara 22 | Umetazamwa mara 30
Download Nota Download MidiMBIU YA UFUFUKO
KIITIKIO
Amefufuka, amefufuka, amefufuka;
Yupo hai mwamba, hafi tena mwamba,
mwamba wa uzima Yesu ameshinda mauti.
Amefufuka, amefufuka, amefufuka;
Kristo amekata kamba za mauti,
ametukomboa mwamba, kaburini hayumo
(Tupige mbiu ya ufufuko, Sauti zivume, Dunia ijue na Mbingu zifurahi kwa upendo mkuu wa kufa na kufufuka Bwana wetu Yesu Kristo,
Tuimbe Aleluya) X 2
MASHAIRI
1a.Jeshi la Malaika wa mbinguni wanafurahi
b.Watumishi wa Bwana duniani tunafurahi
2a.Mkuu wa uzima amefufuka, tushangilie
b.Furahi mama kanisa, tupaze sauti zetu
3a. Nuru ya mwanga wa Kristo wa ufufuko, ituangaze
b. Tufufuke na Bwana wa uzima, tuimarike