Maneno ya wimbo
NGURUMO ZA PASAKA
By Cyprian Alphayo
Utangulizi
Jiwe lile limeviringishwa, limewekwa pembeni, Hofu kuu tetemeko kubwa limetanda kote, na Malaika ameketi upande wa kuume, walinzi wanatetemeka na wale wanawake wapo tayari.
Kutangaza habari njema ya utukufu wa Bwana Yesu, Kutangaza habari njema kwa Kanisa na mataifa ya Dunia yote.
Kiitikio
Ngurumo za nini wapendwa, ni za pasaka, Bwana kafufuka hayumo tena kaburini,
Kishindo cha nini wapendwa, ni cha pasaka, Bwana kafufuka…………………….
Furaha ya nini wapendwa ni ya pasaka, Bwana kafufuka…………………………
Mashairi
1.Patazameni mahali, walipomweka Yesu, Mnazareti aliyesulibiwa amefufuka
2.Kumbukeni alivyosema alipokuwa nanyi Galilaya hayupo amefufuka alivyosema
3.Livunjeni hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu.Maandiko yamtimia Aleluya
Hitimisho
Wakristo, tushangilie tumtukuze Bwana, tumhangilie Mungu kwa makofi, kwa muziki wa shangwe na tupige vigelegele.
Alilili, alilili, Ee-e-e Alililililili
(Tupige Ee-e Makofi Ee-e-e-ee shangilia, furahia)
Bwana amefufuka.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu