Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 545 | Umetazamwa mara 2,456
Download Nota Download MidiKaribuni mezani Bwana awaalika – Enyi wateule wake wote (kwenye karamu) takatifu Bwana ameiandaa, karamu ya kutupatanisha naye
Hivyo basi yatupasa – leo tushiriki hii karamuye
Hivyo basi yatupasa (ndugu) – tushiriki karamuye
Tule mwili tunywe damuye (atualika) Kristu (aliye) Bwana (Mfalme) wetu
Tushiriki heri ya mbingu (atualika) Kristu (aliye) Bwana (Mfalme) wetu
1.Kwa wema wako ee Yesu – kweli watuandalia
Karamu hii takatifu – kweli watuandalia
2.Ndiwe chakula cha mbingu - twajiunga nawe Yesu
Ndiwe kinywaji cha mbingu - twajiunga nawe Yesu
3.Posho yao wasafiri – uzima utupe Bwana
Utuongoze mbinguni – uzima utupe Bwana