Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 775 | Umetazamwa mara 2,394
Download Nota Download Midi1.Twawashangilia hawa wenzetu,
kwa uamuzi wao kuifunga ndoa – Hoye hoye, hoye hoye
Tunawapongeza, tunawatakia heri njema
Ni dhihirisho tosha kweli mwapendana - tunawatakia heri njema
Huu ni mfano bora wa penzi la dhati - tunawatakia heri njema
2.Hii ni siku yenu mliyotengewa,
bwana na bibi harusi mfurahie – Hoye hoye, hoye hoye
Tunawapongeza, tunawatakia heri njema
Mungu awajalie muwe na watoto - tunawatakia heri njema
Na pia muwafunze kumwogopa Mungu - tunawatakia heri njema
3.Bwana harusi umpende mkeo,
nawe bibi harusi umheshimu mumeo – Hoye hoye, hoye hoye
Tunawapongeza, tunawatakia heri njema
Na msameheane panapo makosa - tunawatakia heri njema
Panapo tofauti mtatue kwa amani - tunawatakia heri njema
Uamuzi wenu kweli wapendeza, machoni pa Mungu na viumbe vyake
Mlilolitenda kweli linafaa, dhihirisho tosha kweli mwapendana
Hoye hoye, hoye hoye, hoye hoye, hoye hoye
Tunawatakia heri njema x3