Ingia / Jisajili

Salamu Ee Mama Maria

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 1,254 | Umetazamwa mara 4,885

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1.Salamu ee Mama Maria wanao twakusalimu – Salamu Maria

   Bikira Mama wake Mungu Mama wa Mwokozi wetu – Salamu Maria

Heshima tunazitoa kwako (mstaajabivu) Mama (mpendelevu) sisi tunakusalimu

Kizazi hadi kizazi 'Wewe (mbarikiwa)' kweli (vitataja) sisi tunakusalimu

2.Umebarikiwa Maria Mama umejaa neema –

  Tunakupongeza Mama kutuzalia Mkombozi –

3.Kutaja sifa za Maria mimi kamwe sitaacha –

   Mama usiye na doa Mama usiye nazo dhambi -

4.Kioo cha haki kikao cha hekima mlango wa mbingu -

   Chombo cha neema na heshima chombo bora cha ibada –

5.Malkia uliyezaliwa pasipo dhambi ya asili –

   Afya ya wagonjwa hizo baadhi za sifa zako Mama -


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa