Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 716 | Umetazamwa mara 3,016
Download Nota Download MidiTunawapongeza bwana na bibi harusi
Kwa uamuzi wenu wa kuifunga ndoa
Baraka zake Mungu na ziwashukie
Muishi kwa amani mtunze ndoa yenu
1.Sisi ni mashahidi kwa hii ndoa yenu,
twawaunga mkono kwa uamuzi wenu,
sote tunashiriki kuwashangilia
2.Tunawatakia mafanikio mema,
maisha marefu pia twawatakia,
neema na fadhili zake Mungu Baba
3.Pia watoto wenu wamwogope Mungu,
na muwe kama wa familia takatifu,
ambayo siku zote yampendeza Mungu
4.Penzi lenu liimarike siku zote,
liwe na nguvu lizidi kuwa dhabiti,
penzi lenu liwe imara siku zote